Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:17 am

NEWS: CHAMA CHA CUF CHAFUNGIWA KUFANYA KAMPENI

Chama cha Wananchi CUF Jimbo la Mtwara Mjini kimefungiwa kufanya kampeni kwa siku kumi kuanzia jana Oktoba 10 mwaka 2020 baada ya kulalamikiwa na chama cha Mapinduzi kwa kukiuka kanuni za maadili ya uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa tume ya uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani, Kanali Emanueli Mwaigobeko.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa aliipokea barua kutoka Chama cha Mapinduzi wakilalamikia juu ya ukiukwaji wa maadili ya Uchaguzi wa Rais ,Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 unaofanywa na Chama hicho.

Kamati ya maadili ya Uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini baada ya kupokea barua ya malalamiko siku za nyuma imeketi kikao na kujadili malalamiko hayo ambapo Chama cha CUF kilikili kuyafanya makossa huku wakisema kuwa walifanya hivyo kwa kuwa kuna baadhi ya vyama navyo vinafanya matukio kama hayo.