- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YAWAWEKEA PINGAMIZI WAKINA MDEE
Dar es salaam. Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kimeweka pingamizi katika mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam dhidi ya waliokuwa wanachama wake 19 wa Chama hicho ambao ni wabunge wa viti maalumu, lakini waliovuliwa uanachama wa chama hicho.
Makada hao 19 akiwemo Halima Mdee walifungua maombi ya kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wao, huku chama hicho kikiwasilisha hoja sita.
Pingamizi hilo lilisikilizwa leo Jumatatu Juni 13, 2022 na Jaji John Mgetta, ambaye baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili alipanga kutoa uamuzi wa shauri hilo Juni 22, mwaka huu.
Hata hivyo jopo la mawakili wa Chadema likiongozwa na Peter Kibatala liliwasilisha hoja sita, ambapo hoja moja ilikataliwa dhidi ya wadai hao.
Wabunge hao wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee walifungua maombi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, wakiomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya kuhusi uamuzi huo wa kuvuliwa uanachama.
Sambamba na maombi hayo, pia wamefungua maombi ya zuio la muda dhidi ya ubunge wao kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wao.
Mdee na wenzake walichukua hatua hiyo baada ya uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho, kuwavua uanachama.