- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YATANGAZA KUSIMAMISHA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kusimamisha mgombea katika nafasi ya Urais wa Zanziabar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa leo June 6, 2020 na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar, -Salum Mwalimu huku akiwataka wanachama wa chama hicho wenye sifa na maadili kujitokeza na kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.
Amesema Mwanachama yeyote mwenye nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kuanzia leo anaweza kupeleka barua ya maombi katika mamlaka zinazohusika ndani ya CHADEMA na kwamba zeozi hilo la siku kumi litafika tamati Juni 16 mwaka huu.
Mwalimu ameongeza kuwa milango ipo wazi kwa mwanachama yeyote wa CHADEMA mwenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.
Hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa John Mnyika alitangaza kuwa chama hicho kimefungua milango kwa Mwanachama yeyote mwenye nia ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.