- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YATAKIWA KUJIELEZA KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Francis S. Mutungi amemtaka Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini Chadema John Mnyika kuwasilisha maelezo ya kina ofisini kwake Juu ya Kauli alizodai za kashifa alizotoa dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa hii leo Agosti 12, 2021 na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika kupitia mitandao yake ya kijamii imesema kuwa Jaji Mutungi amedai kuwa kauli za Mnyika zilikuwa ni za kashfa, zenye Lugha Chafu na Kinyume na maadili hapa nchini.
Juzi Agosti 10, 2021 Mnyika aliongea na Vyombo vya habari kama kutoa ufafanuzi baada ya Rais Samia kufanyiwa Mahojiano na Kituo cha BBC, Mnyika alidai kuwa Rais alitoa kauli za uongo kwenye mahojiano yake na Bbcswahili.
RAIS ALIONGEA NINI KUHUSU KESI YA MBOWE.
Agosti 9 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan kupitia idhaa ya kiswahili ya BBC yaliyofanyika Ikulu ya Dar es salaam alisema, uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ulianza Septemba mwaka jana, lakini ulikuwa haujakamilika, alifafanua kuwa mashtaka yake hayakuchochewa kwa sababu za kisiasa.
Mkuu huyo wa nchi alisema anachojua ni kuwa Mbowe alifunguliwa kesi Septemba mwaka jana, akiwa na wengine kwa mashtaka ya ugaidi na uhujumu uchumi.
Hata hivyo, alisema kwa wenzake kesi zao zilishaanza kusikilizwa, lakini Mbowe upelelezi wake ulikuwa haujaisha.
“Tumeingia kwenye uchaguzi, tumemaliza. Sasa polisi wamemaliza uchunguzi wao wamemhitaji kwa ajili ya kuendelea na kazi yao. Lakini kama utakumbuka Mbowe hakuwa nchini kwa kipindi kirefu, alikuwa Nairobi.
“Lakini alivyoingia nchini aliitisha maandamano ya Katiba. Nadhani yalikuwa na mahesabu akijua kuwa ana kesi ya namna hiyo na hii vurugu anayoianzisha, akikamatwa aseme kwa sababu ya Katiba,” alieleza Rais Samia.
MNYIKA ALISEMAJE JUU YA KAULI YA RAIS SAMIA.
Mnyika alisema kuwa, huenda Rais Samia ametoa kauli hizo kwa kuwa alipotoshwa na wasaidizi wake, ambao hawakumuelewesha vyema juu ya Sheria ya Vyama vya Siasa, inayoruhusu vyama hivyo kufanya mikutano ya hadhara na maandamano.
Katibu Mkuu huyo wa Chadema amesema, kwa sasa chama hicho hakitachukua hatua yoyote dhidi ya kauli hiyo, kwani huenda Rais Samia atafuta kauli hiyo.
“Kama wasaidizi wake walikuwa hawajamuonesha kifungu cha 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, juu ya haki ya vyama kufanya mikutano ya hadhara na maandamano. Kama walimpotosha hawakumuonyesha sheria inasemajie, wataenda kumueleza rais haya uliyozungumza hayako kwenye msingi wa kisheria, pengine watatoa muelekeo tofauti,” amesema Mnyika.