- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YAPANGUA HOJA ZA HALIMA MDEE NA WENZAKE
Dar es salaam. Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kimesema kuwa wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho waliovuliwa uwanachama kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama, walikaidi wito wa kwenda kamati kuu ya Chama hicho kwa maksudi.
Chadema imesema mara baada ya wabunge hao kudai kuomba kuongezwa muda wa kuja mbele ya kamati kuu ya chama hicho walielezwa kuwa wanapaswa kufika mbele ya kamati kuu ili kuwasilisha barua hizo za kuomba kuongezewa muda, lakini hawakufanya hivyo.
"walifahamishwa kwa barua kuwa waje mbele ya Kamati Kuu na wawasilishe maombi yao ya kuongeza muda ili Kamati Kuu itafakari na kuona kama inaweza kuwaongezea muda. Badala ya kufanya hivyo waliamua kwa makusudi kukaidi kufanya hivyo" amesema John Mrema Mkurugenzi wa itifaki na mawasiliano wa chama hicho kwenye taarifa yake alioitoa hii leo Desemba 3, 2020.
"Aidha, ifahamike kuwa Kamati Kuu ina mamlaka kwa mujibu wa Kanuni za Chama ibara ya 6.5.1(d) kuchukua hatua za dharura bila kufungwa na masharti ya siku 14 isipokua anayelalamikiwa atakua na haki ya kuitwa kwenye kikao."
Mrema amejibu hoja ya kuwa Kuna baadhi ya Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu ambao walikuwa wanahamasisha Wanachama ili wawafanyie fujo waliokuwa Wanachama 19, napenda kueleza kwamba Chama hakijawahi kuletewa malalamiko yoyote wala ushahidi na waliokuwa wanachama 19 kabla ya kikao hicho kuwa kuna wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama waliokuwa wakihamasisha kwamba wakifika Makao Makuu wafanyiwe fujo.
"Aidha, walipoandika barua kuhusu hofu ya usalama wao, Chama kiliwaelekeza kwamba badala ya kufika Makao Makuu ya Chama kama ilivyokuwa imeelekezwa awali wafike katika Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach ili wawe huru kufika na kujielekeza mbele ya kikao cha Kamati Kuu."
Kwa maana hiyo suala hilo limetumika tu kama kisingizio dhidi ya uamuzi wao wa kukwepa kuja kujitetea mbele ya kikao cha Kamati Kuu.
Kwamba pamoja na nia yao ya kukata rufaa, mpaka sasa Chama hakijapokea rufaa yoyote na kwamba izingatiwe uamuzi wa kuwavua nafasi zao za uongozi ndani ya chama na kuwafukuza uanachama utaendelea kutamalaki na unapaswa kuzingatiwa na wanachama wote na mamlaka zote hadi hapo utakapobatilishwa na Baraza Kuu iwapo wahusika wakikata rufaa na rufaa yao kukubaliwa.