- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CHADEMA YAIANDIKIA TUME BARUA JUU YA RUFAA ZA UBUNGE
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeishutumu vikali Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kutotoa majibu ya rufaa za wagombea wao wa ubunge 16 na za udiwani zaidi ya 300 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara.
Chama hicho kimesema tayari kimeiandikia barua tume hiyo, ikitaka muafaka juu ya majibu ya rufaa za wagombea wake walioenguliwa ‘kinyume’ cha sheria za uchaguzi.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.
“Tangu Agosti 28, mwaka huu, tume imekuwa ikipokea rufaa za wagombea wetu wa ubunge na udiwani waliokuwa wameenguliwa baada ya mapingamizi.
“Tume imepokea rufaa, safari hii nadhani imevunja rekodi haijapata kutokea kwa sababu mwaka 2015 rufaa za udiwani hazikuzidi 71, ubunge zilikuwa 11 nchini nzima.
“Mara hii rufaa ziko mamia na zikaribia maelfu. Chadema peke yetu tulipeleka rufaa za ubunge zaidi ya 49 malalamiko kwa maana ya wale ambao hawakupewa fomu za rufaa na za udiwani zilikuwa zaidi ya 600.
“Hadi sasa rufaa za wagombea 16 wa ubunge wa Chadema hazijatolewa uamuzi na za udiwani ni zaidi ya 300, zimebaki siku 35 watu wapige kura.
“Tayari tumeiandikia barua tume kuhusu wasimamizi wao wanaovunja sheria ili wasiendelee kubariki, hatutaruhusu sheria zivunjwe na kanuni zikiukwe kwa sababu ya kuwapendelea wagombea wa vyama fulani,”alisema.