Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:14 pm

NEWS: CCM YAMTAKA MBUNGE ANAYETAKA KULIPWA KWA DOLA AHAME NCHI.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, amemtaka Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga, kuhama nchini na kwenda nchi wanakulipa mishahara ya wabunge kwa kutumia fedha za Kidolla , huku akimsihi kuwa kama anataka kuhudumia wananchi wake basi afuate utaratibu uliopo hapa nchini.

“Aende kwa hao wanaolipa kwa dola. Kwa nini anafanya kazi hapa? Yupo Tanzania anataka kufanya kazi hapa ya kuhudumia wananchi, afuate utaratibu wa nchi. Akitaka dola aende kwenye hiyo nchi ya dola, ahame hapa,” alisema wakati akihojiwa na gazeti la Nipashe jana Juni 23, 2021.

Chongolo alipoulizwa kama ni wakati sahihi kwa mbunge kusimama bungeni kuomba nyongeza ya mshahara na posho, Chongolo alisema: "Hoja hapo ni mbunge kutaka kulipwa kwa dola, hivyo uwe wakati sahihi au siyo sahihi, aende huko wanakolipa kwa dola."

Juzi Mbunge huyo wa Mbongwe alidai bungeni kuwa wao wabunge wamekuwa wakipitia kipindi kigumu sana nyakati za uchaguzi lakini wamekuwa wakilipwa mishahara na posho ndogo

“Mitandaoni tumekuwa tukitukanwa sana kuwa tunalipwa na hela yetu haikatwi kodi, wamesahau kuwa mpaka huyu kuitwa Mbunge amepitia njia gani, vilevile huyu Mbunge anafuatwa na Watu wangapi, ukiangalia mshahara wa Mbunge ni Mil 3.8”— Maganga, Mbunge wa Mbogwe