- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: CAG ASSAD AWAJIA JUU VIONGOZI WAFUATA UPEPO
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), nchini Tanzania Profesa Mussa Assad amesema kunawatu walikuwa wanaunga mkono matendo ya uvunjwaji wa kisheria na leo watu hao hao wanashadilia mambo ambayo ni kinyume na yale walikuwa wakiyaunga mkono kitendo ambacho Assad amekiita kuwa watu hao ni wasaka fursa na wafuata upepo.
Prof. Assad alitolea mfano kitendo cha Rais aliyepita cha kutumbuliwa kwa watendaji bila hata kufuata sheria na haki za anayetumbuliwa akisema watu walishangilia na kulikuza na sasa hao hao wanashangilia mpaka leo wakati wanapaswa kukosoa mambo yanapokwenda kinyume.
Profesa Assad amesema hayo leo Jumamosi Aprili 10, 2021 katika uzinduzi wa mfululizo wa midahalo ya umma itakayokuwa ikiandaliwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).
“Kuna watu waliunga mkono na sasa wanaunga mkono tena vitu ambavyo haviendani, hao ni wasaka fursa tu na kawaida yao hawatusaidii chochote, nchi inahiaji watu wenye fikra tunduzi ambao wakati ule walisema kitu kile na sasa wanasema vilevile na wataendelea kufanya mambo sahihi,” amesema Profesa Assad.
Amesema ni jambo la kawada watu kuwa hivyo kwa kuwa binadamu wengi ni wasaka fursa, wanaangalia upepo unaendaje, "wakati ule walikuwa wanashadadia mambo yakifanywa hata bila kufuta taratibu za kisheria na sasa wanashadadia hata mambo ambayo yanatofautiana na yale."
Aidha Assad ametolea ufafanuzi suala la mradi wa Bandari ya Bagamoyo, amesema kuna haja ya Serikali kutoa nyaraka ya mradi huo kuiweka hadharani ili wananchi wasome, waangalie faida na hasara zake na watoe maoni yao kama ni mzuri au mbaya.
“Nashindwa kusema kama mradi ni mzuri au ni mbaya maana hiyo nyaraka sijaiona lakini Serikali ikitoa taarifa, ikaitoa Ikulu tutatoa maoni nami ni mzuri katika eneo hilo la uchambuzi,” amesema Profesa Assad.
Profesa Assad mkaguzi aliyeondolewa madarakani kwa madai ya kumalizika kwa muda wake wa uhudumu mnamo tarehe 4 Novemba, 2019.
Pia Assad Amesema kwa mtazamo wake asilimia 60 au 50 ya viongozi ndani ya Serikali sio wazuri, hivyo wanapaswa kupumzishwa ili mambo yaanze upya.
“Viongozi wengi sio wazuri au hawakidhi kiwango kinachohitajika, tatizo langu ni moja tu inapofika mahali unaona mtu anakosea na huwezi kusema kama mtu anakosea, unakuwa umefika mahali pabaya sana,” alisema Profesa Assad na kuongeza:
“Sio lazima umkosoe wazi wazi, lakini angalau basi andika kwamba mheshimiwa nimeona umefanya jambo hili na hili, lakini nafikiri kimsingi jambo hilo halikuwa sawa; rai yangu turekebishe hapa na hapa, akipata rai kwa mtu mmoja atakasirika, akipata rai hiyo kwa watu 10 kwenye cabinet (baraza) yake lazima asikilize”
Amesema tatizo ni kwamba watu wote wamekuwa waoga; imefika mahali watu wengine wananyamaza tu.
“Ndiyo maana nasema tuanze upya tuanze na hao wachache ambao wanakwenda vizuri, hilo pia ni somo kwamba ambao nao ‘in the future’ (baadaye) watakuwa wa ovyoovyo, dawa yao ni hiyo ya kuwaweka kando na kuanza upya,”amesema.
Bunge lakataa kufanya kazi na (CAG) Assad
Bunge la Tanzania halikuvutiwa na kauli ya CAG Profesa Musa Assad wakati katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York mwezi Disemba 2018, alisema kuwa Bunge hilo la Tanzania halina meno na hivyo limeshindwa kuiwajibisha ipasavyo serikali.
Mvutano mkali ulizuka baina yake na Bunge la taifa kufuatia kauli yake hiyo.
Mnamo Aprili mwaka huu Bunge la Tanzania liliazimia kutofanya kazi na CAG huyo anayeondoka Prof Musa Assad, baada ya kumtia hatiani kwa tuhuma za kukidharau chombo hicho cha taifa.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alionyesha wazi kukerwa kwa namna ambavyo Assad hakujutia kauli yake iliodaiwa kuwa ya dharau dhidi ya Bunge la Tanzania.