- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BURUNDI YATOA HATI YA KUKAMATWA KIONGOZI WA UPINZANI
Serekali ya Bunjumbura nchini Burundi imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani wa chama cha MSD nchini humo aliye uhamishoni nchini Ubelgiji Bw. Alexis Sinduhije, ikimtuhumu kwa kuongoza kundi linalohusika na vitendo kadhaa vya kigaidi.
Taarifa hiyo imetolea na Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Burundi Sylvestre Nyandwi Jumatano usiku baada ya msururu wa mashambulizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki katika siku za karibuni, ambapo watu sita walipoteza maisha na zaidi ya mia moja kujeruhiwa.
Lakini hati hiyo inahusiana na mashambulizi ya awali, pamoja na milipuko ya mabomu na uvamizi ambapo dazeni ya watu waliuawa na kujeruhi wengine zaidi ya 100 tangu mwanzoni mwa mwaka 2020, mwanasheria mkuu alisema.
Uchunguzi uliofanywa tayari umebaini kuwa vitendo hivi vimefanywa na kundi la magaidi waklongozwa na Alexis Sinduhije, alidai.
Chini ya sheria ya kitaifa na kimataifa, vitendo hivi ni vitendo vya ugaidi, na pia uhalifu dhidi ya ubinadamu. "
Rais wa chama cha upinzani cha Movement for Solidarity and Development (MSD), Alexis Sinduhije anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji.