- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BUNGE LAKANUSHA WABUNGE KULAZIMISHWA KUCHANJWA CHANJO
Dodoma. Ofisi ya Bunge imekanusha vikali taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya Habari nchini zikidai kuwa kunaulazima wa wabunge wote kuchomwa chanjo ya Corona na kwamba wabunge ambao hawatachanja chanjo hiyo hawataruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa bungeni.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Agosti 14, 2021 na ofisi ya Bunge hilo la Jamhuri imeeleza kuwa taarifa hizo niupotoshaji na hazina ukweli wowote.
“Tunapenda kuujulisha umma kwamba, taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani maelekezo yaliyopo na ambayo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akisisitiza na kuwahimiza wabunge kujitokeza kuchanja chanjo hiyo kwa hiari yao,” imesema taarifa hiyo.
Lakini hata hivyo Ofisi hiyo ya Bunge imesema imeandaa utaratibu utakaowawezesha Wabunge wote kupata chanjo hiyo katika viwanja vya Bunge kwa hiari yao wenyewe.
Wabunge wamesisitizwa kutumia hiyari hiyo kujitokeza ili kupata chanjo kwa ajili ya kujikinga na kuwakinga wengine katika gonjwa hilo.