Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 1:11 pm

NEWS: BUNGE LA URUSI LAIDHINISHA UNYAKUZI WA MAJIMBO MANNE YA UKRAINE

Baraza la Seneti la Bunge la Urusi leo Jumunne limepiga kura ya kuidhinisha mikoa minne ya Ukraine iliyojimegea kuwa sehemu ya Russia, na kusukuma hasira kwa Ukraine na washirika wake wa magharibi na Marekani.

Majimbo hayo manne ya Ukraine ni Luhansk, Donesk, Zaporizhzia na Kherson.

Duma ratifies agreements to recognize 4 regions as Russian territory - CGTN

Shirika la habari la Urusi, TASS limeripoti kuwa Baraza la Shirikisho lilipiga kura ya umoja wa kupitisha muswada wa kuyaunganisha majimbo hayo kwenye Shirikisho la Urusi.

Hatua ilielezewa na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kama “hatari ya kusambaa kwa mzozo” na kwamba mchakato huo hauna nguvu ya kisheria.

Bunge la Russia lilikuwa tayari limeshaidhinisha baada ya Russia kuandaa kura ya maoni katika mikoa minne ya Ukraine inayokaliwa na wanajeshi wa Russia.

Ukraine ilisema kura hiyo ilifanyika chini ya mazingira ya kulazimishwa na haiwakilishi utashi wa raia wa Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson.

Wiki iliyopita, Guterres alisema “kuchukuliwa kwa eneo la nchi na nchi nyingine kwa kutumia vitisho au nguvu ni ukiukaji wa kanuni za mkataba wa Umoja wa mataifa na sheria za kimataifa.”

Huku Russia ikiendelea na mchakato wa madai ya kunyakuwa maeneo ya Ukraine, vikosi vya Ukraine vilichukua tena udhibiti wa maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na Russia.