Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 6:51 am

NEWS: BUNGE LA BURUNDI LAMUIDHINISHA MAKAMU RAIS NA WAZIRI MKUU

Bunge la mchini Burundi jana Jumanne limeidhinisha uteuzi wa wakuu wawili wa nchi hiyo ambao ni makamu rais na waziri mkuu, ambao walipendekezwa na rais mpya, Evariste Ndayishimiye.

Prosper Bazombanza kutoka chama cha UPRONA aliidhinishwa kama makamu rais kwa kura 91, huku wabunge wawili wakikosa kumuunga mkono na mmoja mmoja kutopiga kura

Naye Alain-Guillaume Bunyoni, afisa mwenye cheo cha juu sana katika polisi ya taifa hilo, ambaye ni waziri wa usalama wa muda mrefu wa serekali inayoondoka madarakani, alipitishwa kwa jumla ya kura 94 za wabunge, kama Waziri mkuu mpya.

Cheo cha Waziri Mkuu ni kipya, kwa mujibu wa katiba mpya ya Burundi. Katiba hiyo pia imeondoa cheo cha mmoja wa makamu wa rais, kwani katiba ya zamani ilitambua makamu wawili wa rais.

Bazombanza aliwahi kuhudumu kama makamu wa kwanza wa rais chini ya uongozi wa rais wa zamani aliyefariki, Pierre Nkurunziza, kuanzia mwaka wa 2014 hadi 2015.

Bunyoni yupo chini ya vikwazo vya Marekani na umoja wa ulaya kwa tuhuma za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, wakati wa maandamano ya April 2015, ya kupinga muhula wa tatu wa Rais Nkurunziza.