Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:52 pm

NEWS: BOSSI SHIRIKIA LA NDEGE NCHINI AHUKUMIWA MIAKA 4 JELA

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege nchini Tanzania (ATCL), David Mataka amehukumiwa kutumikia miaka minne (4) jela au kulipa faini ya Tsh milioni 8 mara baada ya kukutwa na hatia katika mashtaka yaliyokuwa yakimkabili yeye pamoja na wenzake.

Hukumu hiyo imetolewa hii leo Ijumaa, Agosti 20, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega katika Mahakama ya Kisutu.

Aidha Mahakama hiyo imewahukumu watuhumiwa wenzake ambao ni Ramadhani Mlinga Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), na aliyekuwa Mwanasheria wa Mamlaka hiyo, Bertha Soka kifungo cha mwaka mmoja ama kulipa faini ya Tsh milioni 2 kila mmoja.

Mataka na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka sita likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 71.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi zaidi ya 20 na vielelezo, Mataka na wenzake wamelipa pesa na kuachiwa huru.