- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOSS MKUU TIGO AITAKA POLISI KURUDISHA PASI YAKE YA KUSAFIRIA
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania anayemaliza muda wake mwanzoni mwa mwezi ujao, Simon Karikari ameliandikia barua Jeshi la Polisi nchini akiliomba kumrudishia HATI yake ya kusafiria.
Katika barua yake hiyo ya Septemba 13, mwaka huu ameeleza kuwa nyaraka hizo zilichukuliwa tangu Februari 6 mwaka huu.
Karikari ameongeza kuwa kibali chake cha kuishi na kufanya kazi nchini Tanzania kinafikia ukomo Oktoba 1 mwaka huu. Amebainisha kwamba nyaraka zilizochukuliwa na ameiomba Polisi kumrejeshea ni pasi zake za kusafiria mbili, moja ya Uingereza na nyingine ya Ghana.
Hatua ya Karikari kuondoka inakuja muda mchache mara baada ya Bossi wa kampuni shindani ya Vodacom Bw. Hesham Hendi kutangaza kuachana na Vodacom mara baada ya kupata kazi nyingine nchini Hispania.
Taarifa ya kuondoka Karikari ilitangazwa Septemba 7 mwaka huu na mwenyekiti wa bodi ya Tigo Ami Mpungwe.