- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BOND ZA BILION 1.5 ZIMENUNULIWA DODOMA.
DODOMA: Baadhi ya Wakandarasi, Wafanyabiashara na Viongozi mbalimbali wa Serikali wamenunua bond zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 kwenye Samia infrastructure bond mapema leo Jumatatu Desemba 16, 2024 Jijini Dodoma.
Bond hii ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya barabara zilizo chini ya wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) zimenunuliwa wakati wa semina ya mauzo ya hatifungani ya Samia Infrastructure bond iliyoratibiwa na Bank ya CRDB.
Akiongoza tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi huo na Mikoa ya jirani kutumia fursa ya hatifungani ya miundombinu ya Samia kwa kujenga barabara imara na zitakazokamilika kwa wakati ili kurahisisha shughuli za maendeleo kwa wananchi.
''Wananchi wenzangu wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa jirani tuitumie fursa hii kushirikiana na Watanzania wenzetu kujenga barabara imara, nazitakazokamilika kwa wakati ili tupite sisi , tusafirishe mazao yetu, nakusambaza bidhaa na huduma zitakazodharishwa kwaajili ya kila mmoja wetu, niwakaribishe wakulima kuweza kununua bondi hizi , nawakaribishe wakandarasi, wafanyabiashara , watumishi, Taasisi za serikali ambazo malengo yake niyakufanya biashara,"
Aidha, Senyamule amesema elimu ya fedha kwa Watanzania wengi bado ni changamoto nakuendelea kuwasisitiza TARURA na CRDB kazi ya kuelimisha jamii kuhusu ununuzi wa bondi hisa iendelee kwa kasi kubwa ili kuhakikisha watanzania wengi wanatumia fursa hii kufaidika na Samia infrastructure bond na kushiriki kuchangia miundombinu ya nchi yao.