Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:46 am

NEWS: BENKI YA EQUITY YAANZA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA WHATSAPP

Nairobi. BENKI ya Equity nchini Kenya imeanzisha mfumo mpya wa utoaji huduma kidijitali katika juhudi za kurahisishia wateja wake mchakato wa kupata huduma za kifedha kwa kutumia njia za WhatsApp na Facebook.

Mfumo huo mpya kwa jina Equity Virtual Assistant (EVA) utawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za benki kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp, Facebook Messenger na Telegram.

Teknolojia hiyo itakayotumika kutoa huduma za benki na usaidizi kwa wateja itawafaidi wateja wa zamani na wale wapya kwa kwa njia ya mawasiliano (chat) na mtumiaji sawia na mawasiliano baina ya marafiki.

Kupitia akaunti zao kwenye mtandao wa EVA, wateja wanaweza kununua vocha ya simu, kutuma hela, kununua bidhaa na huduma, kulipa bili, kutazama salio la pesa pamoja na kupata nakala ya maelezo kuhusu pesa zao wakati wowote popote walipo kupitia mtandao wa kijamii watakaochagua.