- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BAKWATA YATEUA MASHEIKH WA MIKOA 19
Dar es Salaam. Baraza kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) likiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir limefanya uteuzi wa masheikh wakuu wa mikoa 19.
Uteuzi huo wa Masheikh wa mikoa umefanyika kwa mujibu wa katiba ya Baraza hilo, katika kikao kilichofanyika jana Aprili 4, 2021 na wajumbe wa baraza la Maulamaa chini ya mwenyekiti wake Muft Abubakari Zuberi
lakini Uteuzi wa masheikh hao wa mikoa umetangazwa leo Jumatatu Aprili 5, 2021 na msemaji wa Mufti, Khamis Mataka.
Mataka aliwataja miongoni mwa masheikh wa mikoa walioteuliwa ni pamoja na Alhad Mussa Salum ( Dar es Salaam), Shaaban Juma (Arusha), Mustafa Rajab ( Dodoma) na Mohammad Mushangani wa Lindi.
Katika hatua nyingine, Sheikh Mataka amesema Mufti Zubeir amewateua wajumbe tisa wa baraza la Ulamaa ambao ni pamoja na Sheikh Hamid Jongo, Ally Khamis, Shaaban Msuya, Issa Othman na Mkowe Abdallah.