Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 12:54 pm

News: Baada ya kudhalilishwa msanii Odama alipwa zaidi ya milioni 30 na gazeti la udaku la VISA

Dar es salaam: gazeti maarufu nchini limeamuriwa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu kumlipa milioni 30 msaani maarufu wa bongo movie Odama

hukumu hiyo imetolewa mbele ya hakimu mkazi mkuu, Respicius Mwijage, ambea alisema kuwa mahakama hiyo imethibitisha pasi kuwa na shaka, kuwa gazeti hilo la Viza lililenga kumchafua Odama, Hakimu Mwijage alieleza kuwa hukumu hiyo imetolewa baada ya gazeti hilo kuandika kichwa cha habari kikisema '' Odama agawa penzi kwa kinyozi" kichwa hicho cha habari kilichokuwa kinaonesha kumdhalilisha mlalamikaji mbele ya jamii ambapo nikinyuma na sheria za nchi. akaongeza kwa kusema kuwa mapenzi ni swala la mtu binafsi halipaswi kutangazwa mpaka wenyewe wawili wakubaliane kutangaza kwa jamii.