- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AWESO AWATUPA NDANI MAAFISA WA WIZARA TANGA
Waziri wa Maji Juma Aweso ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Tanga kuwaweka ndani watu watatu akiwemo mkandarasi aliyepewa kandarasi ya Zaidi shilingi milioni 600 zilizotengwa kwa ajili ya kukamilisha mradi wa bwawa la maji la kata ya Kwemkambala Wilayani handeni Mkoani Tanga kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha hizo.
Aweso amesema baada ya kulalamikiwa na Wananchi na Wahusika kushindwa kumpa maelezo sahihi ya matumizi ya fedha hizo amewachukulia hatua waliohusika na ubadhirifu wa fedha hizo ambao ni Mtaalamu wa mabwawa kutoka Wizara ya maji, Mdhibiti ubora wa wizara hiyo pamoja na Mkandarasi wa mradi huo.
"Serikali inayoongozwa na Rais samia haiwezi kuvumilia uzembe wa aina hii mnasema fedha zimetumika kumlipa Mkandarasi na hapa hakuna kazi inayoonekana OCD wachukue hao wakatoe maelezo sahihi".
Waziri amesema fedha hizo zilipelekwa mahususi ili Wananchi wa eneo hilo waweze kupata maji safi na kuwaondolea adha hiyo ambayo inawabili kuanzia mwaka 2018.