- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU GWAJIMA NA JERRY SILAA WAVULIWA UJUMBE WA KAMATI YA BUNGE
Dodoma. Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima na Mwenzake wa jimbo la Ukonga Jerry Silaa wamevuliwa Ujumbe kwenye Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge waliokuwa wakihuduma kama wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya wawili hao kuwa kwenye tuhuma za Kusema Uongo na Kulidhalilisha Bunge.
Juzi Spika Wa Bunge Job Ndugai aliwaita wabunge hao kwenda kwenye kamati hiyo kwaajili ya kujibu tuhuma zao zinazowakabili za kusema Uongo na Kushusha hadhi na Heshima ya Bunge.
Gwajima alianza kuhojiwa jana na kamati hiyo kwa zaidi ya saa mbili na kesho ataendelea kuhojiwa, huku Silaa naye anahijiwa leo mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Emmanuel Mwakasaka.
Kwa mujibu wa Mwakasaka, kamati hiyo ina jumla ya wajumbe 24 wakiwamo Gwajima na Silaa na sasa imebaki na wajumbe 22.
“Unapotuhumiwa mara nyingi, wewe ndio mshtakiwa zipo taratibu zinafuata. Kama wewe ni mtuhumiwa huwezi kuwa hakimu kwenye kesi yako mwenyewe,” alisema.
Alipoulizwa ni lini waliondoka katika ujumbe wa kamati hiyo, Mwakasaka alisema: “Ninapozungumza na ninyi hawa (Silaa na Gwajima) si wajumbe wa kamati hii.”
Kuhusu kama wanaweza kurejeshwa kwenye kamati, mwenyekiti huyo alisema wanaweza iwapo Spika (Job Ndugai) atataka kufanya hivyo kwa sababu ndiye anayeteua wajumbe wa kamati.
Hata hivyo, alisema hawezi kulizungumzia jambo hilo kwa kina kwa sababu mwenye mamlaka ya kuwarejesha ni Spika wa Bunge kwa kuwa liko ndani ya madaraka yake.
Jumamosi wiki iliyopita Spika Ndugai aliamuru Gwajima na Silaa wapelekwe kwenye kamati hiyo, ili kujibu tuhuma zinazowakabili.
Gwajima alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo jana wakati Silaa atatakiwa kufika kwenye kamati hiyo leo saa 7.00 mchana