Home | Terms & Conditions | Help

April 3, 2025, 12:01 pm

NEWS: ASKARI WAWILI WAFARIKI DUNIA WAKIJIBIZANA KWA RISASI NA MHALIFU

MPWAPWA: Askari wawili wa wameuawa katika Kijiji Msagali Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wakati wakipambana kumkamata mtuhumiwa wa unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Kwa mjibu wa Taarifa iliyotewa leo tarehe 18 Disemba, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP-George Katabazi imesema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya Saa Saba wakati Askari hao ambao ni D/cpl. Jairo Boniphace Kalanda na pc Alfred John wakiwa katika mapambano ya risasi baada ya kufika nyumbani kwa kusindikizana na Mwenyekiti wa Kijiji kwa lengo la kutaka kumkamata mtuhumiwa aitwaye Atanasio Malenda (30) Mkulima Mkazi wa Kijiji hicho aliyekuwa akituhumiwa kumjeruhi na kumpora Yohana Lameck kiasi cha Shilingi Milioni mbili.

"Askari Polisi hao wakiwa na wenzao walipata taarifa kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akitafutwa yuko nyumbani kwake katika kijiji cha Msagali na walifika kijijini hapo na kuutafuta uongozi wa kijiji na kuelekea nao nyumbani kwa mtuhumiwa huyo. mtuhumiwa huyo alitoka ndani na kuanza kuwashambulia askari na katika majibizano hayo ndipo vikatokea vifo hivyo" imesema Taarifa ya Kamanda Katabazi

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo naye amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpwapwa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapambano hayo.