Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 2:01 am

NEWS: ANUANI ZA MAKAZI KUWEKWA KWA MIEZI 5

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali imekusudia kutekeleza uwekaji wa mfumo wa anuani za makazi kwa muda wa miezi mitano badala ya miaka mitano kama ilivyokuwa itekelezwe hapo awali.

Waziri Nape amesema zoezi hilo linafanyika kutokana na misingi mitatu ikiwemo Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umoja wa Posta Duniani (UPU).

Mbunge huyo wa Mtama amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo hakuna mbadala isipokuwa ni kutekeleza kwa nguvu zote kwani Serikali inadhamiria kuwasaidia wananchi kuboresha mawasiliano katika sehemu mbalimbali ikiwemo makazi yao, sehemu zao za biashara na maeneo mengine ya huduma za kijamii.

Aidha, Waziri Nape amesema utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi ni jambo la kihistoria ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuacha alama kwa watanzania na lengo lake ni kurahisisha mawasiliano na kuifanya jamii kuwa ya kisasa zaidi bila kusahau kuimarisha ulinzi katika makazi yao.