Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 1:43 am

NEWS: ALIPWA MILIONI 1.7 KUMTONGOZA NA KUMUUA MWANAMKE

Dar es salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam leo Januari 25, 2022 limesema linawashikilia Watu wawili wanaodaiwa kula njama na kisha kumuua Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Barke Pesa Rashid (30) ambaye ni mkazi wa Ilala Utete Jijini Dar es salaam, Kwa madai ya kwamba Mwanamke huyo aligharamiwa na Mwanaume matumizi mbalimbali hadi kumpangishia nyumba ya kulala lakini akawa anachepuka na Wanaume wengine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Jumanne Januari 25, 2022 na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Murilo amesema kuwa Tukio hilo limetokea January Mosi,2022 Tabata Segerea kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Maridadi ambako tarehe hiyo

"Mtuhumiwa wa kwanza Mwanaume, Jonsiner Bounser( 34), Mkazi wa Segerea Kalabash Pub alifanya mipango ya mapenzi na Mwanamke aliyemuua baada ya kula njama na Mtuhumiwa mwingine wa pili aliyekamatwa Mwanaume anayeitwa White (33) Mfanyabiashara ya Lori la kuzolea taka Mkazi wa Tabata Segerea"

"Mwanamke huyo alikabwa shingo mpaka kupoteza maisha akiwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni, Bounser alikodiwa na White kwa malipo ya Tsh.Milioni 1.7 ili amtongoze na baadaye aende kumuua Mwanamke huyo kwa madai kuwa White alimgharamia sana na kumpangishia nyumba lakini Mwanamke huyo ana Wanaume wengine"

"Bounser amekiri kupewa Tsh. Milioni 1.2 kwa nyakati tofauti kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo na kwamba alikuwa bado anadai Tsh. Laki tano kwa White kwa mauaji ya Mwanamke huyo, uchunguzi wa tukio hilo unakamilishwa na watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo" amesema Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam