Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 10:04 pm

NEWS: ALIKIBA AKIMBIWA NA WASANII WAKE WAWILI WA KINGMUSIC

Wanamuziki wawili waliokuwa wakisimamiwa na lebal ya Muziki ya kings music records inayosimamiwa na Msanii AliKiba, Cheed na Killy wamejitoa katika Lebal hiyo na Kuamua kufanya kazi zao binafsi.

Uwamuzi huo wameutangaza kwa pamoja usiku wa kuamkia leo kupitia mitandao yao ya kijamii.

Wasanii hao chipukizi Kila mmoja aliandika Maneno sawa na aliyoandika mwenzie kwenye mitandao yao ya kijmiii na sehemu pekee walipoachana kwenye muandiko ni kwenye kuweka jina lao tu.

"Napenda kuwajulisha fans wangu watu wangu wote waliokuwa wakisupport mziki wangu na wanaoendelea kussuport kazi zangu na hata wasiosupport pia ni kwamba kuanzia leo hii napenda kutamka kuwa mimi sio tena msanii wa kingsmusicrecords nimeamua hili kwa akili yangu timamu kabisa bila kushawishiwa na mtu wa aina yeyote ile na sijatumia kilevi chochote kile ni maamuzi yangu tu binafsi na ni kwa ajili ya muendelezo wa mziki wangu"- waliandika Wasanii hao

Pia wasanii hao walitoa shukrani zao za dhati kwa aliyekuwa Boss Wao Alikiba

"Alikiba amekuwa ni mtu muhimu sana kwenye maisha yangu amekuwa ni mtu ambae amenionyesha njia na kuniaminisha mimi pamoja na mziki wangu mbele ya jamii Inshallah mwenyezi mungu amlipe kwa kila alichonifanyia na kujitolea kwa ajili ya mziki wangu namshkuru sana sana sana nasitoacha kumshkuru siku zote za maisha yangu naumia ila sina budi alikiba nakupenda sana my brother nakupenda mnooo na unajua hilo"

"Cha zaidi napenda nikushkuru kwa kunielewa nikiwa kama mdogo wako bado nahitaji baraka zako bado ntahitaji support kutoka kwako kwa namna moja ama nyingine ama kwa kile ambacho kitakuwa na umuhimu kuwa supported na ningeomba pia uniombee dua safari yangu iwe njema na yenye mafanikio popote pale ntakapokuwa as long as najua hatujaachana kwa ubaya na wala hatujawahi kuwa na ugomvi labda NO" waliandika Wasanii hao.