- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT YAPIGA KIPENGA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI
Dar es salaam. Chama cha Upinzani cha ACTwazalendo kimetangaza Rasmi tarehe ya Kuchukua, kujaza na Kurejesha fomu za kugombea katika nafasi mbali mbali za Uongozi(Ubunge, Udiwani na Urais).
Kwa mujibu wa Taarifa ya Chama hicho iliyotolewa mchana wa leo Juni 22, 2020 imesema kuwa Zoezi la Kuchukua, Kujaza na Kurejesha fomu katika chama hicho litafanyika kuanzia Julai 1 mpaka Julai 13 mwaka huu.
Chama kimewatahadharisha wanachama na wagombea wake juu ya vitendo vya Rushwa katika mchakato wa Kuchukua na Kurejesha fomu za kuwania nafasi ya uongozi.
"ACT Wazalendo haitamvumilia mwanachama yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa kwenye zoezi la uteuzi wa wagombea wake." - amesema Ado Shaibu Katibu mkuu wa chama cha ACT Wazalendo.