- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT YAJIUNGA SEREKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR
Dar es Salaam. Chama Kikuu chenye ushawishi mkubwa visiwani Zanzibar cha ACT Wazalendo kimeridhia takwa la kikatiba la kujiunga kwenye Serekali ya Umoja wa kitaifa viziwani humo Mara baada ya kuapata Zaidi ya Asilimia 12 ya kura zote kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 27 na 28 mwaka huu.
Tangazo hilo limetolewa leo hii Desemba 6, 2020 na katibu mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kuketi jana Jijini Dar es salaam.
Kikao cha kamati kuu kimeielekeza Kamati ya Uongozi ya chama hicho kupendekeza jina la mwanachama atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar haraka.
Pia, imeazimia kuwaruhusu Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani wa chama hicho waliochaguliwa kwenda kukiwakilisha chama na wananchi waliowachagua.
Akisoma maazimio hayo, Ado amesema; “Mosi kamati kuu ya chama chetu imeazimia wawakilishi wachache kwa maana ya madiwani, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge ambao wametangazwa kushinda waruhusiwe kushiriki kwenye vyombo vyao vya uwakilishi,” amesema Ado na kuongeza
“Pili Kamati Kuu ya chama chetu imeridhia chama kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na imeielekeza Kamati ya Uongozi ya chama chetu kupendekeza jina la mwanachama atakayekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,” amesema Ado akisoma maazimio ya kamati kuu ya chama hicho.
Amesema kuwa chama hicho kimefikia uamuzi huo kutokana na kupata mawazo ya kuwasikiliza wanachama na viongozi wa chama hicho