- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT WAZALENDO WAPIGWA BARUA NA MSAJILI, WATAKIWA KUJIELEZA
Dar es Salaam. Chama cha Upinzani cha ACT Wazalendo kimeandikiwa barua na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kikitakiwa kujieleze ni kwa nini kisichukuliwe hatua za kisheria baada ya Mwenyekiti wake, Maalim Seif Sharif Hamad kupanda jukwaa la mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu katika mkutano uliofanyika Moshi mjini Oktoba 19, 2020
Akizungumza na gazeti la Mwananchi hii leo Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alikiri ofisi hiyo kuipatia ACT barua hiyo.
Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 22, 2020 na Mwananchi, Naibu Katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Joran Bashange amekiri kupokea barua hiyo na amesema wanaijibu. “Ni kweli tumepokea barua, kosa letu ni mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kusimama jukwaa la mgombea mwingine,” amesema Bashange.
Pia, amesema barua hiyo inahoji ni kwa nini mikutano ya ACT Wazalendo inahudhuriwa na viongozi wa vyama vingine na wa dini wanaowaunga mkono. “Sheria ya vyama vya siasa iko wazi inasema, mtu anapovunja sheria anahukumiwa, yaani ahukumiwe na mahakama, sasa yeye anatafsiri anataka atupe adhabu, adhabu gani? aende mahakamani,” amesema Bashange