Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:30 am

NEWS: ACT WATANGAZA MRITHI WA MAALIM SEIF

Chama cha Upinzania cha ACT Wazalendo nchini Tanzaia kimesema tayari kimeshapitisha jina la mtu atakaye shika wadhfa wa Makamu wa kwanza wa Rais visiwani Zanzibar.

Tangazo la chama hicho limetolewa leo hii na Kiongozi mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe wakati wa kisomo cha kumuombea Marehemu Mwenyekiti wa Chama hicho Maalim Seif.

Tangazo hilo limetokana na vikao vya ndani vya Chama vilivyoanza Siku ya Ijumaa Februari 26, 2021 kwa ajili ya kupitia majina na hatimaye kuchagua jina moja la Othuman Masoud ambaye atarithi nafasi ya Maalim Seif aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.

Kiti cha makamu wa kwanza wa rais Zanzibar kiliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho na mwanasiasa mkongwe, Maalim Seif Sharif Hamad, kufariki dunia mnamo Februari 17. Mwaka huu.

Kikao hicho kilikutanisha vigogo wa chama hicho kupitia kamati ya uongozi chini ya kiongozi wake mkuu, Zitto Kabwe.

Kikao cha mwisho kimefanyika mchana wa Jana jijini Dar es Salaam kilifanyika kukiwa kumesalia siku tano tu, kabla ya tarehe ya mwisho ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais kutimia kama inavyoelekezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na katika mabadiliko yaliyofanyika mwaka 2010, ambayo inatoa siku 14 baada ya mtu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuondoka.

Miongoni mwa majina yaliyokuwa yanapendekezwa ni pamoja mwanasiasa wa siku nyingi na mwenye uzoefu wa muda mrefu wa vyama vya upinzani, Haji Duni Haji, maarufu kama Babu Duni. Yeye ndiye makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo visiwani Zanzibar na anatajwa kwa uhodari wake wa kujenga hoja wakati anaposhiriki mijadala ya aina mbalimbali. Akiwa amezaliwa Novemba 26,1950 alikuwa miongoni mwa mawaziri waliofanya vyema wakati ilipoundwa serikali ya kwanza ya umoja wa kitaifa katika mwaka 2010 hadi 2015.

Kando na yeye, jina la Nassor Ahmed Mazrui linachomoza katika kinyang'anyiro hicho na anaelezewa kama mtu anayekubalika ndani ya chama na hata nje yake. Akiwa amezaliwa mwaka 1960, naye pia amewahi kuwa sehemu ya baraza la mawaziri katika serikali ya awali ya Umoja wa Kitaifa iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Ali Mohammed Shein.

Na Jina lingine likawa ni Othman Masoud Othman.. Licha ya kutokujinasibisha hadharani kuwa sehemu ya vyama vya upinzani, Masoud anatambuliwa kwa msimamo wake usioyumba wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani na nje ya nchi na pia uwezo wake mkubwa kwenye taaluma yake ya sheria.