Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 8:14 am

NEWS: ACT KUTAFUTA MRITHI WA MAALIM SEIF JANUARI 29

Dar es salaam. Chama cha ACT Wazalendokimetangaza kufanyika Mkutano wake Mkuu Maalumu mwezi Janauri 29, 2022 ukiwa na lengo la kufanya Uchaguzi wa M/kiti wa Chama hicho Taifa.

Mkutano huo utahudhuriwa na Viongozi wa Vyama kutoka mataifa mbali mbali kama Zimbabwe, Zambia, DR Congo, Malawi, Uganda na Kenya.

Taarifa ya mkutano huo maalum imetolewa na kiongozi mkuu wa chama hicho Ztto Kabwe hii leo Desemba 23, 2021 kupitia ukurasa wake wa twitter.

"Ninafarijika kuona kuwa Mkutano wetu Mkuu wenye wajumbe zaidi ya 700 unafadhiliwa na Wanachama wa ACT Wazalendo kutoka Majimbo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano. Hakika Chama ni Wanachama. Tumefanya vikao vyote vya kikatiba vya Chama kwa michango ya Wanachama" alimesema Zitto.

Sambamba na hilo Zitto amesema kuwa siku moja kabla ya kufanyika kwa mkutano huo chama hicho kimepanga kuzindua mfumo wa kadi ya kidijitali ya uwanachama ili kila mwanachama wa chama hicho awe na kadi ya kieletroniki.

ACT Wazalendo kitakuwa chama cha 3 baada ya chama tawala CCM na Chadema kuanzisha mfumo kama huo wa kusajili wanachama kidijitali, ikiwa ni hatua ambayo itasaidia kuingiza mapato kwa urahisi, kujua idadi sahihi ya wanachama.

Imeandikwa na Deyssa H. Deyssa, Muakilishi Publisher. Na imehaririwa na Merry Mgawe