Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 1:41 am

NEWS: ACCACIA WAONDOLEWA KWENYE SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

Dar es Salaam. Kamapuni ya Madini ya ACCACIA leo Novemba 18, 2019 inaondolewa kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) ikiwa ni utekelezaji wa taarifa ya kampuni hiyo kwa wadau wake ya Septemba 17 kuwa hisa zake zote zilizokuwa zinamiliki Accacia zimenunuliwa na Barrick Gold Corporation.

Kabla ya mauzo hayo, Kampuni ya Barrick ilikuwa inamiliki hisa asilimia 63.9 na wanahisa wengine wakiwa na asilimia 36.1 zilizobaki.

Kampuni ya Accacia ina miaka minane ya kudumu katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), tangu kuorodheshwa kwake

Kampuni hiyo, iliyoorodheshwa DSE Desemba 2011 ikijulikana kama African Barrick Gold (ABG) kabla haijabadili jina na kuitwa Acacia Novemba 2014, inaondolewa sokoni hapo baada ya kukamilisha utaratibu wa kufutwa.

“Acacia ilifutwa katika Soko la Hisa London (LSEG) tangu Septemba. DSE itaifuta kuanzia leo, Novemba 18, 2019,” inasomeka taarifa ya DSE iliyowekwa kwenye tovuti yake.

Kufutwa kwa kampuni hiyo, taarifa zinaonyesha kutapunguza ukubwa wa mtaji wa soko hilo kutoka Sh19.67 trilioni uliokuwapo mwishoni mwa wiki iliyopita hadi Sh16.94 trilioni.

Wakati ukubwa wa mtaji wa soko zima ukipungua, ule wa kampuni za ndani, Sh9.01 trilioni, hautabadilika.

“Hii inamaanisha ndio mwisho wa kuwa na kampuni ya Acacia katika soko letu. Walituandikia nasi tumewakubalia kuwafuta,” alisema Moremi Marwa alipozungumza na gazeti la mwananchi jana.