- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
Newas: Waziri wa Mazingira wa Burundi apigwa risasi na kufariki Dunia
BUJUMBURA: WAZIRI wa Mazingira wa Burundi aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa njiani kwenda nyumbani kwake wakati wa mkesha wa mwaka mpya amefariki akiwa na umri wa miaka 54
Emmanuel Niyonkuru, 54, aliuawa muda wa saa 00.45 kwa saa za Afrika ya Kati na “jambazi aliyekuwa na silaha,” msemaji wa polisi aliandika kwa njia ya Twitter.
Pierre Nkurikiye kwa Twitter alisema kwamba mwanamke ambaye alikuwa na Niyonkuru amekamatwa kwa ajili ya kuhojiwa, kutokana na mauaji hayo.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alisema kwamba mhusika wa kosa hilo lazima aadhibiwe.
Mamia ya watu, wakiwemo maafisa wa ngazi za juu wa jeshi, wameuawa katika machafuko toka Rais Nkurunziza agombee muhula wa tatu mwaka 2015, kitu ambacho wapinzani wake walidai kuwa ni kinyume na katiba ya nchi hiyo. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri aliyeko madarakani kuuawa.
Kwa miezi kadhaa sasa nchi hiyo imekuwa katika hali ya utulivu.