- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NCCR: HATUYATAMBUI MATOKEO YA UCHAGUZI
Mkuu wa Idara ya Uenezi na mahusiano ya umma Taifa ndugu Edward Julius Simbeye, amesema NCCR-Mageuzi ikiwa ni moja ya chama cha siasa kilichoshiriki uchaguzi, akiyatambui matokeo ya uchaguzi huo kama matokeo halali bali ni matokeo batili kutokana na mchakato wake kuwa wa hovyo na usiofuata taratibu za uchaguzi.
Simbeye amesema kumefanyika hujuma kubwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia kwenye vituo vya kupigia kura hivyo kufanya hata matokeo yake kuwa ni batili.
“Nchi yetu imemaliza mchakato wa uchaguzi ambao ulikuwa na makandokando mengi sana ambayo kimsingi yamevuruga uchaguzi wenyewe na kupelekea uchaguzi wenyewe kutokuwa halali”
“Msimamo wa chama chetu ni kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, matokeo ya uchaguzi hayawezi kuwa halali kwa sababu mchakato wote wa uchaguzi ulikuwa na matatizo ya kutofuata kanuni na sheria tulizojiwekea