- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NAPE: TCRA SITISHENI KUPANDA KWA VIFURUSHI VYA SIM
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nnauye Nape ameiagiza mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA kuyaamuru makampuni yote ya simu nchini kusitisha upandishaji wa bei mpya ya Vifurushi mpaka hapo Mitandao hiyo itakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo.
Mbunge huyo wa jimbo Mtama amesema kuwa ameanza kusikia wananchi kuanza kulalamikia bei za vifurushi vya simu kupanda ghalfa tena kwa bei kubwa huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa hata kiwango cha vifurushi wanchopewa wakinunua hakiendani na bei hali wanayokuwa wamekatwa.
"Upandaji wa bei za vifurushi limekuwa kama tatizo sugu ambapo mitandao ya simu hupandisha, lakini wakielekezwa na Serikali wanashusha bei, baada ya muda wanapandisha tena.
Agizo Nape amelitoa Jana Januari 20, 2022 visiwani Zanzibar wakati akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ujenzi wa minara 42 ya mawasiliano katika shehia 38 itakayojengwa katika visiwa vya Pemba na Unguja.
Wakati anazungumza kuhusiana na ujenzi wa minara hiyo pia akazungumzia umuhimu wa mawasiliano.