Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:08 pm

NAIBU SPIKA ACKSON: SUGU HAJANIKABIDHI OFISI MPAKA SASA

Mbunge mpya wa jimbo la Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson, amesema Hajakabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu hadi sasa hivi.

Ackson amesema kuwa hakuna chochote kilichofanyika kati yake na mtangulizi wake huyo aliyekuwa anatumia Ofisi za Ardhi Mbeya.

"Hadi sasa hakuna makabidhiano na mbunge mstaafu, Joseph Mbilinyi, siwezi kumlazimisha, mimi nimejiandaa kikamilifu kuwatumikia wananchi siwezi kusubiri kwa sababu naona hajihusishi na chochote na ni mlolongo mrefu, ndiyo maana hata ofisi natumia nyingine", ameongeza Dkt.Tulia.

Tulia ambaye ni Naibu Spika wa Tanzania ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari hii leo Novemba 23, 2020 wakati akitangaza kuwa ameanza utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi.

Dkt Tulia amesema kila Alhamisi atakuwa anasikiliza kero mbalimbali katika ofisi yake iliyoko kwa mkuu wa wilaya ya Mbeya na kila Jumamosi atakuwa kwenye ofisi zake zilizopo Uyole.