Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 1:24 am

MWIGULU: WAFANYABIASHARA WEKENI FEDHA BANKI, HAZITACHUKULIWA

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango hapa nchini, Mwigulu Nchemba amewasihi wafanyabiashara kuacha tabia ya kuficha pesa zao majumbani kwao, kwa hofu ya kuchukuliwa fedha hizo na Serekali na badala yake waweke banki kwa usalama zaidi.

Mbunge huyo wa Iramba Magharibi ametoa kauli hiyo hii leo Jumamosi Aprili 3, 2021 katika kikao na watendaji wa wizara hiyo na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) na Msajili wa Hazina (TR).

Waziri huyo mpya wa fedha amesema kuwa katika fedha zitakazowekwa benki serekali itachukua sehemu tu ya kodi yake na si vinginevyo.

"Kwa wale wafanyabiashara walioona wakiweka fedha zao zitaonekana mtandaoni labda zitachukuliwa zote nitoe rai warudishe fedha kwenye mabenki zitaliwa mchwa au panya bila sababu, uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi.”

“Kodi itatozwa tu kwa sehemu ya fedha inayotakiwa kukusanywa na sisi tujenge utaratibu wa kutii sheria kulipa kodi na kuwa wazalendo kwa nchi yetu.” Amesema Mwigulu.

TAFAKURI

Kauli ya Mwigulu Nchemba inakuja siku 6 kupita mara baada ya Rais wa sasa wa Tanzania Samia Suluhu Hassani siku ya Tarehe 28.3.2021 kuwaonya Watendaji wa Serikali kuacha tabia ya kutumia nguvu kukusanya kodi, kufungia biashara zao, kunyang'anya fedha kwenye akaunti kisa Sheria inawaruhusu.

akaongezea kuwa Kitendo hicho kinasababisha wafanyabiashara kufunga biashara zao na kukimbilia nchi Jirani na hatimaye Serikali kukosa mapato.