Home | Terms & Conditions | Help

May 19, 2024, 12:40 am

MWASITI: MAMA YAKE GODZILLA ALINAMBIA NIMSAIDIE MWANAE ATOKE KIMUZIKI

Msanii wa Bongo fleva Mwasiti Almasi Nyangasa(Mwasiti), ameweka wazi kuwa alishawahi kufuatwa na mama mzazi wa marehemu Godzilla akimtaka amsaidie, ili naye afanikiwe.

Mwasiti ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba kutokana na jambo hilo akawa karibu sana na familia ya Godzilla, na kushirikiana kwenye masuala mbali mbali ya kijamii.

“Ilikuwa benki mjini, Godzilla alikuwa amekuja na mama yake, akaniambia napenda unavyoimba, ningependa pia umshike mkono mdogo wako na yeye aishi katika mazingira mazuri na kufanya kazi, nikamwmabia sawa, mama, kuanzia hapo tukawa karibu sana kama familia, tulikuwa tunaongea mambo mengi sana”, amesema Masiti.

Ukaribu wa Mwasiti na Godzilla ulipelekea watu kuwahusisha kutoka kimapenzi na walikuwa na mpango wa kutoa alibamu ya pamoja.

Godzilla amefariki dunia juzi Februari 13, na anatarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi, Februari 16 katika makaburi ya Kinondoni.