- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MWANASHERIA MKUU: NIMELIPOKEA SWALA LA WATUMISHI KUCHAPWA VIBOKO
Dar es salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Prof. Adelardus Kilangi amesema Ofisi yake imepokea malalamiko mengi juu ufafanuzi wa uchapwaji wa viboko hadharani ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya viongozi wa umma kwa wananchi na baadhi ya watunishi.
Prof Kilangi ametoa kauli hiyi Jana Januari 2, 2021 alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mkazi wa Mtwara, Muba kwenye kipindi cha Papo kwa Papo kinachoendeshwa na Mbunge, Humphrey Polepole kila siku za Jumamosi katika kituo cha chama cha mapinduzi cha Channel Ten.
Muba aliuliza swali kuwa “Kumekuwa na tatizo hili limekuwa likiendelea sijajua limekaaje kidogo, kwa sababu sawa viongozi wetu wanafanya kazi nzuri hatukatai, lakini sasa kutandikwa viboko mbele ya kadamnasi na vyombo vya habari kidogo inakuwa changamoto, nikasema nipige simu kutoa dukuduku langu, je hili limekaaje?,”
Akijibu swali hilo, Prof. Kilangi amesema “Nakushukuru sana kwa jambo hilo, na mimi nimelisikia pia na wananchi kadhaa wameniletea, sisi wajibu wetu kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni kutoa ushauri wa kisheria kwa serikali, viongozi na taasisi mbalimbali ikiwemo tafasri ya sheria na kueleza sheria inasema nini katika masuala mbalimbali.
“Japo wakati mwingine tunapotimiza majukumu yetu huwa hatuelezi kwamba tumetoa ushauri gani katika jambo husika, kwani wakati mwingine huwa ni kuelewa tu sheria inasema nini au inataka nini katika jambo husika.
“Katika hilo niseme tumelipokea rasmi kama serikali na kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tutalifanyia kazi kwa mujibu wa majukumu yetu kama tulivyokabidhiwa kikatiba na kwa sheria zilizotungwa na bunge,” amesema Prof. Kilangi.