- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MUSWADA: KUKUTWA NA BANGI HATA KIDOGO NI KOSA LA JINAI
Bunge la Tanzania limepitisha Muswada wa Sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na 5) ya mwaka 2021 ambao unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria tisa za Tanzania kwa lengo la kuboresha baadhi ya masharti katika Sheria hizo na kuondoa mapungufu yaliyobainika wakati wa utekelezaji wake tangu kupitishwa kwake.
Moja ya marekebisho yaliyopendekezwa kwenye Muswada huo ni marekebisho katika Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ambapo kifungu cha 17 kinarekebishwa ili sasa iwe ni kosa la jinai kwa Mtu kukutwa au kutumia hata kiwango kidogo cha dawa za kulevya kama vile heroine, bangi na mirungi kwani kabla ya marekebisho haya Sheria ilikua inazuia tu kitendo hicho lakini haikuwa inaeleza kama ni kosa la jinai.
"Vifungu namba 15 na 15(a) vya sheria ya dawa za kulevya vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza uzito wa bangi na mirungi anayoweza kukutwa nayo Mtu katika makosa yanayosikilizwa Mahakama Kuu, ya Hakimu Mkazi au ya Wilaya" alisema Mwanasheria Mkuu Prof. Kilangi.