- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MO DEWJI : CHAMA HAENDI POPOTE ANAMKATABA NA SIMBA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Club ya Simba Mohamed Dewji amesema kuwa Mchezaji wa Club hiyo Clatous Chama hatakwenda kokote kwasababu kwasasa wameshamalizana nae na anamkataba wa miaka miwili na club hiyo.
Mo ambaye pia ni Mwekezaji wa Club ya Simba ametoa ufafanuzi huo hii leo Novemba 15, 2020 wakati akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
“Simba tumejipanga, Chama hajaenda popote, tushasaini nae mkataba atabaki na Simba hadi 2022 kwa hiyo hoja ya Chama tuimalize. Tumemalizana na Chama na ni mchezaji halali wa Simba”-Mohamed Dewji
“Chama anamapenzi na Simba na ni mchezaji mzuri ambaye ameshakuwa mchezaji bora wa Ligi na ameshinda tuzo nyingine nyingi. Hatuwezi kuruhusu watu watuwahi.”
“Chama tulishamalizananae muda mrefu lakini hatukutaka kutangaza, tulitaka kuja kutangaza rasmi lakini kuna propaganda zimezidi kwa hiyo tunataka kuwatuliza mashabiki wa Simba ndio maana tumetoka na kutangaza.”
“Hatuwezi kutamka kiasi gani tumemlipa kwa sababu tumekubaliana hatutasema sehemu yoyote, kwa hiyo nikisema kesho Chama anaweza kuipeleka Simba mahakamani kwa sababu imekiuka makubaliano.”