- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MNYIKA: LAZARO NA METHEW NI WASALITI WAMEJIONGEZA
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa kikuu cha Upinzani nchini Chadema, John Mnyika amesema kitendo cha waliokuwa makada wa chama chao(Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew) kuhama na kurejea CCM ni kitendo cha kisaliti na wamefanya kujiongeza kwakuwa wameshindwa kupambana mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi Mnyika ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibamba na Ubungo amefafanua kuwa chama hicho kilifahamu kuwa Lazaro Nyalandu na Seleman Mathew, ambao wote walikuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama chao, wangeondoka kutokana na mienendo yao waliyokuwa wakiionyesha kwa siku za hivi karibuni.
“Hawa ni wasaliti, wamejiongeza wameshindwa kuvumilia baada ya mateso ya kuporwa ushindi wa ubunge mwaka 2020. Chadema itasonga mbele hadi mabadiliko, uhuru na haki na demokrasia vipatikane nchini.
Mnyika amesema kuwa nafasi zao ndani ya chama hicho yatazibwa na watu mahiri wapambanaji
“Mapengo yao yatazibwa na makamanda wengine na mapambano yanaendelea,” alisema Mnyika