- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MNYIKA: CHADEMA HAIJATEUA MAJINA YA WABUNGE VITI MAALUM NA HATUJAPELEKA ORODHA YA MAJINA NEC
Katibu mkuu wa chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania cha Chadema John Mnyika amesema chama chao hakijateua majina ya wabunge wa viti maalum mpaka sasa na hakuna orodha kutoka ofisi ya katibu mkuu wa chama iliyokwenda tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Ufafanuzi huo ameutoa hii leo Novemba 24, 2020 kupitia mtandao wa twitter mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kwamba Chama hicho kimeshateua Majina ya wabunge wa viti maaalum na wanataka kuyawasilisha kwenye tume ya Uchaguzi.
Mnyika amedokeza kuwa amepata taaatifa kuwa Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC inataka kughushi saini na Orodha ya Majina ili ifanye uteuzi na Bunge kubariki majina hayo.
Aidha Mbunge huyo wa zamani wa Kibamba amesema kuwa wanaendelea kufuatilia kila haatua ya ofisi ya Bunge
"Tunafuatilia yanayojiri ofisi ya Spika Bunge na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua" amesema Mnyika.
Kisheria Chadema wanatakiwa kuwa na idadi ya wabunge 19 mara baada ya kupata zaidi ya Asilimia 12 ya idadi ya kura alizopata mgombea wa Urais wa Tanzania Tundu Lissu kwenye uchaguzi uliofanyika Octoba 28 mwaka huu.
Lissu ambaye ni Makamu mwenyekiti wa chama hicho aligoma kuyakubali matokeo ya uchaguzi huo siku moja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kupiga kura.
Uchaguzi wa Octoba 28 ulipigwa vikali na wapinzani wengi kutokana na kugubikwa na madhila ya ubadhirifu na Wizi wa kura uliodaiwa kufanywa na chama tawala cha CCM.
Wadau wengi wa siasa nchini Tanzania wamekuwa na maoni mfanano juu ya uchaguzi huo wengi wao wakioneshwa kutoridhika na mchakato mzima wa uchaguzi kutokana na chama tawala kutumia vyombo vya dola katika kila hatua ya uchaguzi.
Uchaguzi wa Octoba 28 uliacha watu weingi midomo wazi mara baaada ya kushuhudiwa takribani wapinzani wote kuangushwa katika majimbo yao hali ambayo haijawahi kutokea tangu tuingia kwenye chaguzi za vyama vingi vya kisiasa mwaka 1995.