Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 8:38 pm

MBOWE: SIJAGOMBEA URAIS KWASABABU NATAKA KUKIJENGA CHAMA ZAIDI

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kuwa anaheshimu uwamuzi na ushauri aliopewa na wazee wa chama hicho kumtaka atie niya ya kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi ujao Octoba 2020.

Mbowe amesema kuwa anataka kutumia muda wake mwingi katika kukijenga na kukiimarisha chama hicho.

Amesema kuwa anaamini wagombea waliojitokeza katika nafasi hiyo wote wanafaa kuongoza taifa la Tanzania na anaamini wapo wengine wameshafikisha barua kwa katibu za kutia nia ila hawajajitangaza.

"Wagombea ambao wameshajitokeza mpaka hatua ya sasa, nina imani kabisa ni wagombea wazuri, ni wagombea bora na bado nina imani wapo wagombea wengine wengi ambao ni bora"

"Sikukusudia kutia nia katika nafasi ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sio kwa sababu siwezi ila ni kwa sababu nina amini katika kutumia muda wangu zaidi kujenga Taasisi, kukijenga Chama na kunyanyua vipaji vya Uongozi miongoni mwa vijana, Wazee, Wamama na hata wasichana miongoni mwao"

Nimekitumikia Chama hiki tangu kimezaliwa kwa unyenyekevu na uadilifu mkubwa kwa zaidi ya miaka 30. Umri wangu ni Chama hiki, muda wangu wote wa ujana nimeutumia katika harakati.

Sasa hili ombi lenu Waheshimiwa Sana Wazee wangu, sisi kama Chama tuliweka utaratibu kwamba siku ya leo (jana)Juni 15 ndio iwe siku ya mwisho ya kutangaza nia.

Natambua wako ambao wametangaza nia hadharani, wako ambao hawajatangaza hadharani, lakini wamewasilisha barua zao za makusudio kwa Katibu Mkuu, wote hawa ni wa kwetu, na wote hawa Chama kwa kutumia mifumo yake itawapima na kuhakikisha mwisho wa siku anapatikana mwakilishi ambae wote waliotangaza nia watamuunga mkono.

Mimi kama Mwenyekiti sitakubali na sitaruhusu katika hatua yoyote ya sasa, Chama hiki tukagawane makundi ya wagombea wa Urais. Hatua ya kujitokeza wagombea wengi ni hatua za awali za kuwezesha ndoto za kila mmoja wetu kutimia.

Yawezekana ukawa na ndoto hiyo, wenzako wakakwambia bado kidogo usubiri, kwa hiyo yoyote ambae hatimaye atatolewa kama chaguo la Chama, wajibu wake mkubwa sio kupeperusha bendera ya kundi lake, ni kuunganisha wote wale waliogombea hatimaye wataungana pamoja na wale ambao hata hawakugombea ili twende katika uchaguzi wa Oktoba tukiwa Chama kamili, Chama imara, Chama chenye mshikamano.