- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MBOWE: HATUWATAMBUI WABUNGE 19 WA VITI MAALUMU
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania (Chadema), Freeman Mbowe amesema chama chake hakijawahi kuteua wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chama hicho na wamepanga kusikiliza rufaa za wabunge hao tarehe 25 Aprili, 2022.
Aidha Mbowe ameongezea kuwa Spika wa Bunge ameshaandikiwa barua na anajua wabunge 19 wa viti maalumu sio wabunge walioteuliwa na chama hicho.
Mbowe amesema hayo leo Ijumaa Machi 18, 2022 jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Machi 16.
Amesema Baraza Kuu litakaa mwezi ujao tarehe 25 na kama kuna rufaa zao tutaziona.
“Chadema haijawahi kuteua Kamati Kuu na ninarudia tena leo Chadema haijawahi kuteua wabunge wa viti maalumu” amesema Mbowe
Mbowe pia ametaja mambo matatu aliyozungumza na Rais Samia baada ya kutoka Maahabusu.
Freeman Mbowe ametaja mambo matatu waliyozungumza na Rais Samia Suluhu Hassan walipokutana Machi 4, 2022 baada ya kutoka gerezani, ikiwamo kujadili njia bora ya kutafuta amani na suluhisho katika kufanya siasa.
Amesema; “Tulikubaliana aache kuzungumzia neno amani azungumze neno haki. Jambo la tatu nilimfahamisha yeye apende au mtu mwingine Chadema ni Chama Kikuu cha Upinzani huwezi kukiacha nje.”
Akisisitiza kuhusu hoja hiyo, amesema chama hicho kipo kila mahali na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vingine haviwezi kuinyamazisha.
“Mambo mengine Nilimwambia tutazungumza baada ya kukutana na chama changu,” amesema.