- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAREKANI NA ISRAEL ZA SAINI HATI YA KUIZUIA IRAN KUUNDA NYUKLIA
Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Yair Lapid wamesaini ahadi ya pamoja ya kuizuia Iran kuunda silaha za nyuklia.
Viongozi hao wawili wametia saini maazimio hayo baada ya kufanya kikao cha pamoja magharibi wa Jerusalem katika siku ya pili ya zaira ya rais Joe Biden katika mataifa ya mashariki ya kati.
Akizungumza na televisheni ya Israel mjini Jerusalem, Biden amesema anaunga mkono uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran, kama chaguo la mwisho.
Kauli yake hiyo inachukuliwa kama kuridhia wito wa Israel kuyataka mataifa yenye nguvu duniani kuifanya Iran ijue bayana kuwa inakabiliwa na kitisho dhahiri cha kivita.
Soma pia:Mazungumzo ya mkataba wa nyuklia na Iran mbioni kuanza tena
Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani ameshikilia msimamo wa utawala wake wa kutaka kufufua makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, mchakato unaopingwa vikali na Israel.
Mtangulizi wa Biden, Donald Trump aliiondoa Marekani katika makubaliano hayo ya mwaka 2015, uamuzi ambao Biden amesema haukuwa wa busara.
''Nadhani lilikuwa kosa kubwa sana kwa rais wa zamani kujiondoa katika makubaliano yale." Alisema Biden na kuongeza Iran iko karibu zaidi kupata silaha za nyuklia kuliko wakati mwingine.
"Haihusiani na ikiwa kikosi cha walinzi wa mapinduzi kitaendelea na shughuli zake au la" alisema na kusisitiza kuwa hilo lunaweza kulishughulikiwa wakati huo huo kukawa na makubaliano ya kuudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.
Kikosi maalum cha Iran katika orodha ya magaidi Marekani
Walinzi wa mapinduzi ni kikosi maalumu katika jeshi la Iran, ambacho Marekani imekiweka kwenye orodha ya magaidi, Biden amesema hatakubali shinikizo la Iran kukiondoa kwenye orodha hiyo, hata kama hilo linamaanisha kutofikiwa kwa makubaliano mapya