- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAKALA: JUKUMU LA KILA MTU ULINZI WA MTOTO.
WAKATI dunia ikiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Takwimu za mwaka 2020 zimebaini kuwa katika wilaya ya Chamwino idadi ya waliofanyiwa vitendo vya ukatili ni 439 miongoni mwao wakiwemo wasichana wenye umri chini ya miaka 19 waliokeketwa.
Vilevile Takwimu za huduma za afya ya uzazi katika wilaya hiyo iliyo sehemu ya wilaya 7 zinazounda mkoa wa Dodoma zinaeleza kuwa kati ya wajawazito 14,900 waliojifungua katika mwaka 2020 wajawazito 3438 ni wasichana walio na umri chini ya miaka 18.
Katika wilaya ya Singida Mjini suala la upatikanaji wa Takwimu za matendo ya Ukatili inatajwa kuwa changamoto ambapo katika kipindi kama hicho (yaani mwaka 2020) ni kesi saba pekee zilizotolewa taarifa zikijumuisha tatu za ubakaji na nne za ndoa za utotoni ambapo Afisa ustawi wa jamii Raphael Tilihongelwa anasema Takwimu hizo haziendani na uhalisia katika wilaya hiyo iliyopo mkoani Singida.
Takwimu hizo zimetolewa Wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Katika Mikoa ya Singida na Dodoma yaliyoandaliwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la ACTIONAID TANZANIA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo AFNET,MEDO, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jeshi la Polisi, JUWACHA, SAPAWA, Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Chamwino.
Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na watoto wilaya ya Chamwino Neema Mlula, amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia katika wilaya hiyo bado vimeshamiri na hivyo zinahitajika hatua za maksudi katika kuvikabili.
Uwepo wa madawati ya jinsia katika vituo vya jeshi la polisi nchini ni ishara kuwa mapambano ya ukatili yanahitaji nguvu ya pamoja huku akieleza kesi nyingi chanzo ni wazazi kutokuwa karibu na watoto wao na ikitokea wanamaliza kimila Askari wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Chamwino Nabwike Wilson amesema.
Kwa upande wao wananchi akiwamo Shida Hamisi amakazi wa Iringa Mvumi Mkoani Dodoma waonyeshwa kusikishwa na baadhi ya viongozi wa dini kushiriki kufungisha ndoa bila kuhoji umri,nakuwaomba kuhakikisha kuwa kila wanapofungisha ndoa wapate vyeti vya kuzaliwa vya wanandoa huku wakitoa angalizo kwa wazazi na walezi kuwa makini katika kuwaangalia watoto ikiwamo kuondoa tabia hatarishi zinazochochea mazingira ya ukatili.
Afisa kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Florence Chaki, ametoa wito kwa wakazi wa Mikoa ya Singida na Dodoma kujitokeza kutoa malalamiko yao pindi wanapoona haki yao inapotea.
Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyoangazia maeneo Makuu Matatu Ukeketaji, Ndoa za Utotoni na Mimba za Utotoni yamefanyika katika kijiji Cha Nzali kata ya Chilonwa , Iringa Mvumi , Manchali wilayani Chamwino Mkoani Dodoma na Kijiji cha Merya , Mgori , Kijota Wilaya ya Singida DC Mkoa wa Singida, na kuratibiwa Shirika la Actionaid Tanzania.