- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAKALA: Je unamfaham Malcolm X. ? moja ya watu walio pigania haki za watu weusi nchini Marekani
Honolulu; Leo nakuletea historia ya moja ya mtu maarufu ulimwengu aliyekuwa mpigania haki za binaadamu hususani za watu weusi nchini Marekani na Duniani kwa ujumla wake.
Malcolm X alizaliwa kama Malcolm Little Mei 19, 1925 huko Omaha, Nebraska. Baba yake, Earl Little alikuwa mchungaji asiyeogopa kusema ukweli, na pia alikuwa msaada mkubwa sana wa kiongozi wa Harakati za Weusi (Black Nationalist) wakati huo, Marcus Garvey. Malcolm X alilelewa katika imani ya kisabato na mama yake.
Maisha ya Malcolm mwanzoni yalikumbwa na masaibu mengi. Kwa mfano, mwaka 1929 nyumba yao iliyopo Lansing, Michigan ilichomwa moto na kundi la wazungu lenye chuki; alikuwa na umri wa miaka sita tu wakati baba yake alipokufa katika kifo kibaya sana; mama yake akawekwa katika hospitali ya watu wenye matatizo ya akili (mtindio wa ubongo); akachukuliwa kwenda kulelewa katika vituo vya kulelea watoto wasio na uwezo; mwalimu wake alivunja ndoto zake za kuwa mwanasheria, alimwambia kazi hiyo haiendani na maniga (weusi), akamuusia awe fundi seremala akimsisitiza hata Yesu alikuwa seremala. Akaacha shule japokuwa alionesha ana uwezo mkubwa wa akili; akatumia sasa muda wake mwingi Boston, Massachusetts kufanya kazi za ajabu ajabu; japokuwa kazi yake ya mwanzo ilikuwa kung’arisha viatu; akasafiri kuhamia Harlem, New York ambapo akafanya uhalifu sana; kabla ya mwaka 1942, alikuwa mwongozaji vikundi vya madawa ya kulevya, umalaya, ukahaba, na kamari; na ilipofika mwaka 1946, alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 10 kutokana na kukutwa na kosa la ujambazi (wizi wa kuvunja nyumba).
Malcolm X alijiongezea elimu yake wakati yuko jela. Ilikuwa humo humo gerezani ndio ambapo aliimezaDictionary (aliihifadhi kichwani kamusi ya kiengereza yote), alisoma Biblia na kila kitu kuanzia somo linalohusu mabaki ya kale (Archeology) mpaka Somo la Uzazi na Kurithiana (Genetics). Wakati yupo humo gerezani, Malcolm akafata imani ya muislam mweusi na baada ya kuachiwa kutoka gerezani, akawa mjumbe katika Chama cha Waislamu Weusi (Nation of Islam) na kuchaguliwa kuwa msemaji wao.Nation of Islam ni kundi lilopotoka linalojinasibisha na Uislamu. Alijitoa toka katika Nation of Islam mwaka 1964 na kuanzisha kengine kiitwacho Muslim Mosque, Inc na pia akaundaChama cha Umoja wa Wamerika Weusi (Organization of Afro-American Unity), kundi ambalo linatetea uzalendo wa watu weusi. Baadhi ya Waislamu wa Kisunni walimuusia sana Malcolm kuusoma Uislam wa kweli. Malcolm X alikubali ushauri ule ambao ukamfanya ajiengue kutoka katika Nation of Islam na baadae kukiri:
“Katika chuo kimoja na kengine ambapo nilipita kuongea katika mikutano isiyo rasmi, wengi kati ya watu weupe wamekuwa wakinifata wakijitambulisha kama waarabu, waMashariki-ya-Kati, au wanatoka kaskazini mwa Afrika na wapo hapa kimasomo, kikazi au wengine wana makazi ya kudumu. Wakawa wananiambia pamoja na maneno yangu ya kuwachukia wazungu, ni kweli sikosei ninavyojichukulia kuwa ni Muislamu lakini walihisi niusome vizuri Uislamu, nitauelewa na kuukubali. Kama mfuasi wa Elijah (kiongozi wa Nation of Islam), nilikasirishwa na walichokuwa wakinisema. Lakini baada ya hali hii kujirudia kwa muda, nikajiuliza mwenyewe, kama kweli mtu yuko kidhati katika kuitangaza na kuifata dini hii, iweje mtu arudi nyuma katika kujiongezea maarifa ya kuijua dini hiyo zaidi na zaidi?!…” -Itaendelea week ijayo
-Itaendelea week ijayo