- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAJALIWA : AJIRA ZIMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 17
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema idadi ya watu walio na ajira nchini imeongezeka kutoka watu milioni 20.5 mwaka 2014 hadi kufikia watu milioni 24.1 mwaka 2020/2021, sawa na ongezeko la asilimia 17.5, ambapo kati yao wanaume ni milioni 12.4 na wanawake ni milioni 11.7.
Waziri Majaliwa amesema katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali kwa upande wake itahakikisha inaongeza kasi ya kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji, utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali zenye lengo la kuwezesha nguvukazi tuliyonayo kuajiriwa na kujiajiri.
Pia ameziagiza Wizara zote zenye dhamana ya ukuzaji ajira kuhakikisha zinaandaa programu na mikakati bora ya ukuzaji ajira ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wadau wote nchini washiriki katika utekelezaji wake ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira
Aidha Waziri Majaliwa amezielekeza Ofisi na wizara zote zenye dhamana za uwekezaji na biashara zihakikishe zinashirikiana na wadau wengine hususan sekta binafsi kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kutoa fursa ya kuanzishwa kwa viwanda vitakazochochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Novemba 24, 2021) wakati akizindua Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Soko la Ajira kutokana na utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2020/2021. Uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar.
Hata hivyo, amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuchambua viashiria vyote na kuhakikisha kuwa inakua na ripoti ya kina itakayowezesha maboresho mbalimbali ya kukuza ajira na uchumi nchini.
Amezipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Ofisi ya Rais - Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar; Ofisi ya Taifa ya Takwimu; Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar pamoja na wadau wa maendeleo kwa kufanikisha Utafiti huo.