- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
LATRA: NAULI HAZIJAPANDA, NI ZILE ZILE
Dar es salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) imekanusha vikali taarifa za ongezeko la nauli kwa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ya Tanzania ambayo yanayoanza safari katika kituo cha mabasi cha Mbezi mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha taifa cha Runinga cha TBC, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Gewe amewataka Wananchi kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zinazodai kupanda kwa nauli hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Mustafa Mwalongo amesema hakuna nauli iliyoongezeka.
Pamoja na Mamlaka za LATRA kukanusha lakini yapo manung'uniko kutoka kwa baadhi ya Abari ambao wemeelezea kupanda kwa nauli kinyemela.
Yusufu Ndiola msafiri kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya amesema "nauli imepanda kiana sema tu watu hawafuatilii lakini mi nimekuja hapa nimekuta kunaongezeko la Tsh. 5,000 mpaka sehemu nyingine elf 10"