Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:57 pm

KOREA KASKAZINI IMESEMA HAINA MPANGO KUFANYA MAZUNGMZO NA MAREKANI

Taifa Korofi la Korea Kaskazini limesema halina mpango tena wa hivi karibuni wa kuendelea na mazungumzo baina yake na nchini ya Marekani. Ni mazungumzo hayo ni yale yanayoitaka nchi hiyo kusitisha mpango wake wa kuboresha Makombora ya nyuklia.

Vietnam Hanoi | Treffen Kim Jong-Un und Donald Trump (picture-alliance/AP Photo/E. Vucci)

Mazungumzo hayo ni yale yanayolenga kuitaka Korea ya kaskazini iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia. Akizungumza kupitia shirika la habari la taifa la Korea Kaskazini, naibu wa kwanza wa waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Choe Son Hui amesema leo 04.07.2020 kuwa, nchi yake haioni uhitaji wowote wa kukutana na Marekani.

Nordkorea Kim Jong Un (picture-alliance/AP Images/KCNA)

Choe ameyasema hayo wakati alipokuwa akijibu minong'ono kuwa mkutano mwingine kati ya Raisi wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un, utafanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwezi Novemba mwaka huu.

Raisi wa Korea Kusini Moon Jae alipendekezwa tena kuwa mpatanishi katika mazungumzo hayo. Kwa mujibu wa maafisa wake, wakati wa mkutano kwa njia ya video uliofanyika Jumanne iliyopita, Moon Jae alisema kuwa anataka kufanya kila liwezekanalo kuwakutanisha viongozi hao wa Marekani na Korea Kaskazini kabla ya uchaguzi wa Novemba.