Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 1:57 am

KIKOSI KAZI CHABAINI TUME YA UCHAGUZI SIO HURU

Dar es salaam. Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Profesa Mukandala, amesema kuwa tume zote mbili za uchaguzi NEC na ZEC siyo huru na kwamba wapo baadhi ya watendaji katika tume hizo ambao wanavunja sheria za uchaguzi wazi wazi.

Profesa Mukandala ameeleza hayo hii leo Machi 21, 2022 wakati kikosi kazi kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi ilipokutana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kumkabidhi taarifa ya kikosi kazi hicho. Profesa Mukandala amemshukuru Mhe Rais kwa kukubali kukutana nao ili wamkabidhi ripoti hiyo.

Aidha, Profesa Mukandala ameongeza kwamba wamebaini kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unakuwa mgumu kwasababu unasimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI jambo linalowapelekea baadhi ya wananchi walioandikishwa kupiga kura kutoshiriki kikamilifu na hata kutokupiga kura kabisa, na kwamba kuna haja ya kufanyia marekebisho sheria ya uchaguzi na vyama vya siasa.

Kikosi kazi hicho pia kimepenmdekeza kwamba kuna ulazima wa Tume Ya Uchaguzi kufanyiwa tathimini, lakini pia ufanyike ubainifu kisha mapendekezo ya namna bora ya kuwa na Tume Huru Ya Uchaguzi katika nchi yetu.

Profesa Mukandala amesema kuwa kikosi kazi hicho kimebaini kuwa mchakato wa katiba mpya uliacha baadhi ya mambo ya msingi katika Katiba pendekezwa. Lakini pia kikosi kazi kimependekeza kuwa hakuna haja ya kuwa na katiba mpa kwani katiba iliyopo inaweza kufanyiwa marekebisho.